Maziwa ni kinywaji chenye ladha tamu na muhimu sana kwa afya ya mwili wako, inashauriwa kunywa maziwa walau glass 2 au tatu kwa siku hasa maziwa yaliyo ondolewa mafuta au cream (skimmed milk). Inawezekana una kunywa maziwa lakini ufahamu yanaenda kufanya kazi zipi katika mwili wako Maziwa yana calcium, vitamin A, B 12, D, proteins ambavyo vyote vina faida mwilini kama ifuatavyo;
- Kuimarisha mifupa; maziwa yana calcium na phosphorus ambavyo hufanya mifupa mwilini iwe imara na kuzuia hitilafu katika mifupa.
- Meno imara; maziwa husaidia kuboresha afya na uimara wa meno, kuzuia meno kuoza na kutoboka sababu yana vitamini d, calcium na phosphorus.
- kupunguza uzito, kama utatumia skimmed milk mara kwa mara yanasaidia kuondoa mafuta yasiyo takiwa mwilini ambacho ndio chanzo cha unene.
- Kupunguza msongo wa mawazo/stress, kama una kichwani umetingwa na mawazo hadi au BP inapanda, jaribu kunywa glass ya maziwa ya uvuguvugu utajisikia vizuri, kwenye maziwa kuna kitu kinaitwa lactium inasaidia kutuliza hormones zinazoleta stress.
- Kuzia usipate cancer, maziwa ya ng’ombe yana kitu kinaitwa lactoferrin na inafanya kazi ya chembechembe za cancer zisikue katika mwili wako.
- Maziwa yenyewe yana maji ndani yake hivyo ukinywa inasaidia kuongeza maji mwilini na kusaidia mfumo wa usagaji chakula kufanya kazi vizuri hasa kama una kunywa skimmed milk.
- Watu wanao kunywa Maziwa ( skimmed milk) mara kwa mara maziwa yanasaidia moyo usishambuliwe na magonjwa pia kisukari kupata ni uwezekano mdogo.
- Maziwa yanasaidia kutuliza matatizo ya allergy kwa ngozi, osha ile sehemu ya ngozi iliyopata allergy kwa maziwa kwa kutumia pamba na allergy itapungua.
- maziwa kuboresha ngozi ya uso wako, ukiwa na chunusi, vipele, madoa doa tumia maziwa kusafisha uso wako, chukua kitaulo laini na chovya katika maziwa na sugua uso wako taratibu kisha osha baada ya nusu saa, ukifanya hivyo mara kwa mara matatizo kwenye ngozi yataisha.
- uso ukiwa mkavu au una mikunjo, chukua maziwa kikombe kimoja chanyanya na ndizi iliyosagwa kisha paka usoni kama nusu saa osha, itasaidia ngozi kuwa nyororo ukifanya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment