Michirizi mara nyingi zinatokea tumboni, mapajani, mikononi karibu na mabega, mapajani na saa nyingine kwenye mpaka limo na maziwa. Zinatokea sababu ya ujauzito, kunenepa na mabadiliko mbalimbali yanayo endelea mwilini. Sijui kama kuna mwanamke anayependa kuwa na strech marks maana zinakera
sana.
Unapotaka kuondoa strech marks(Michirizi ) ni vizuri kwanza kujaribu kuzitoa kwa kutumia vitu asilia, ikishindikana ndio unaweza kufikiria kutumia cream,lotion au sabuni vilizotengenezwa viwandani ambazo kama utakuwa na hakika hazina madhara kwa ngozi yako.
1. Aloe vera
Chukua majani ya aloe vera kamua kupata maji yake, kisha unapaka kwenye maeneo yote yenye strech marks, na unaacha kwa dakika 15 kisha unaosha na maji, ukimaliza paka mafuta ya nazi au olive kulainisha ngozi.
2. Ute wa yai
Chukua mayai utakayoona yanatosha kupaka kwenye maeneo yote yenye stretch marks mwilini mwako, kumbuka kutoa kiini cha yai, unapaka ule ute mweupe tu unakoroga vizuri na uma kabla ya kupaka, na baada ya nusu saa osha na maji ya uvuguvugu. Ukimaliza paka mafuta ya nazi/olive
3. Limao/ ndimu na tango
Saga tango kwenye blender kisha chuwa kupata maji yake, yachanganye na maji ya limao kisha paka kwenye maeneo yote yenye stretch marks. Osha na maji ya uvuguvugu baada ya nusu saa, kisha paka mafuta ya nazi/olive. Limao au tango kadiria kiasi kinachokutosha.
Tumia njia moja wapo hapo juu, unaweza kuwa unafanya hivyo jioni au asubuhi kutegemea na nafasi yako. Ila unatakiwa ufanye mara kwa mara au kila siku ili uone matokeo bora , kwa wiki mbili au zaidi. Bidii yako na uvumilivu vinahitajika. Pia ukiwa na strech marks usipende kuacha ngozi yako iwe kavu, paka mafuta ya nazi/au olive mara kwa mara katika mwili isipokuwa usoni, yanasaidia kulainisha ngozi na kuizuia isiendelee kutanuka.
Mazoezi ni muhimu husaidia kupunguza unene ambao husababisha kutokea kwa michirizi.
Vile vile kuzingatia lishe bora na Kunywa maji ya kutosha kila siku.
Toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment