Saturday, November 19, 2016

ZIJUE FAIDA ZA ASALI




image



Asali ni kitu kinachotumiwa na jamii nyingi toka zamani kwa matibabu (afya), ngozi (urembo) na mapishi sababu inasaidia vitu vingi. Ila leo tuangalie faida za kutumia asali kama dawa kwa mambo madogo madogo nyumbani;

  • Tiba ya Allergy
Asali inasaidia sana kuleta nafuu kama ukipata allergy yoyote iwe umekula au umeshika kitu kimekudhuru tumboni au kwenye ngozi, unaweza kulamba vijiko viwili vya asali au ukatia asali kwenye chai ukanywa, au kupaka kwenye ngozi inaleta nafuu.


  • Kuupa mwili nguvu
Asali kama ilivyo sukari inasaidia kuupa mwili nguvu ili uweze kujiendesha tofauti sukari ina madhara ukitumia sana tofauti na asali, hivyo ni vizuri kutumia asali badala ya sukari na ikafanya kazi ile ile bila kuleta madhara kwa afya yako.






  • kupunguza uzito
Ukitaka kupunguza uzito tumia asali kwenye chai za viungo asilia badala ya sukari kama tangawizi,mdalasini, limao, mchaichai itasaidia sana kupunguza uzito kwa haraka.

  • Kutibu kikohozi na matatizo ya koo 
 Unapokuwa na kikohozi au maumivu ya koo na hujapata dawa za hospitali iwe jaribu kula asali  iliyochanganywa na tangawizi iliyosagwa kiasi italeta nafuu, mtoto unaweza kumpa asali kijiko kidogo kimoja mara tatu
.
  • Kuondoa mba kichwani
Asali inasaidia kuondoa mba kwa. Nywele ambazo hazina wekwa relaxer, chukua asali vijiko 5 vya kulia chakula na changanya na vijiko vya maji 2 koroga vizuri, tia nywele maji zilowane kisha paka asali katika ngozi ya kichwa iache mpaka baada ya saa moja osha na maji ya uvuguvugu fanya hivyo mara mbili kila wiki kwa mwezi mzima mba wataisha.









Inashauriwa kutumia asali kwa kiasi hasa watu wenye kisukari, shinikizo la damu ni vizuri kupata ushauri wa daktari. Kama unajua faida nyingine za asali tueleze kwenye comments.



No comments:

Post a Comment