Sunday, November 20, 2016

MAMBO YA KUMFANYIA MPENZI WAKO AZIDI KUKUPENDA



 



Mbusu

Pendelea kumbusu mpenzi wako pale mkiwa pamoja na kumshika mkono mkiwa mnatembea pamoja ,hii humjenga kujiamini kuwa anapendwa .


Fanyika kuwa msaada

Jiweke kipao mbele pale anapopata shida na kumliwaza hii humjenga kuwa kimbilio lake ni wewe anapo pata shida .

Mtoko muhimu

Wanawake hupenda kutolewa out na wapenzi wao hii hupelekea kujiona kama yeye ni wapekee katika hii dunia .

Kuwa muwazi kwake

Jaribu kuwa muazi kwa mpenzi wako ili ajue matatizo yako ,wanawake wengi hupenda kutoa ushauri kwa wale wanaowapenda,hii itamjenga kujiona kuwa anathaminiwa.

Usiwe busy kupiliza

Kuwa busy sana hupelekea migogoro katika mapenzi ,hivo jitahidi hata kumtumia sms mpenzi wako kumjulia hali ukiwa ofisini ili kumtoa wasiwasi.Vizuri zaidi kumuweka wazi kwa busy utakaokuwanao siku iyo.

Mkumbatie

Mkumbatie mpenzi wako mara kwa mara hii huojeza hisia kati yenu na kuzidi kumiss pale mtapokuwa mbali.

Staarabika

Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae.Mwanamke hupenda ustaarabu hasa kwa mtu ambaye anampenda ukizingua mara utamkosa .

Mdekeze

Msichana anapenda kudeka na kubembelezwa sana hivo mvulana ukidekewa usikasirike .Msichana ni kama mtoto kwahiyo jifunze kumbembeleza.





Toa maoni yako.






















   

Saturday, November 19, 2016

KUONDOA MICHIRIZI(STRECH MARKS) KWENYE NGOZI KWA VITU VY ASILIA

   


Michirizi mara nyingi zinatokea tumboni, mapajani, mikononi karibu na mabega, mapajani na saa nyingine kwenye mpaka limo na maziwa. Zinatokea sababu ya ujauzito, kunenepa na mabadiliko mbalimbali yanayo endelea mwilini. Sijui kama kuna mwanamke anayependa kuwa na strech marks maana zinakera 
sana.

Unapotaka kuondoa strech marks(Michirizi ) ni vizuri kwanza kujaribu kuzitoa kwa kutumia vitu asilia, ikishindikana ndio unaweza kufikiria kutumia cream,lotion au sabuni vilizotengenezwa viwandani ambazo kama utakuwa na hakika hazina madhara kwa ngozi yako.

1.  Aloe vera

Chukua majani ya aloe vera kamua kupata maji yake, kisha unapaka kwenye maeneo yote yenye strech marks, na unaacha kwa dakika 15 kisha unaosha na maji, ukimaliza paka mafuta ya nazi au olive kulainisha ngozi.

2. Ute wa yai

Chukua mayai utakayoona yanatosha kupaka kwenye maeneo yote yenye stretch marks mwilini mwako, kumbuka kutoa kiini cha yai, unapaka ule ute mweupe tu unakoroga vizuri na uma kabla ya kupaka, na baada ya nusu saa osha na maji ya uvuguvugu. Ukimaliza paka mafuta ya nazi/olive

3. Limao/ ndimu na tango

Saga tango kwenye blender kisha chuwa kupata maji yake, yachanganye na maji ya limao kisha paka kwenye maeneo yote yenye stretch marks. Osha na maji ya uvuguvugu baada ya nusu saa, kisha paka mafuta ya nazi/olive. Limao au tango kadiria kiasi kinachokutosha.

Tumia njia moja wapo hapo juu, unaweza kuwa unafanya hivyo jioni au asubuhi kutegemea na nafasi yako. Ila unatakiwa ufanye mara kwa mara au kila siku ili uone matokeo bora , kwa wiki mbili au zaidi. Bidii yako na uvumilivu vinahitajika. Pia ukiwa na strech marks usipende kuacha ngozi yako iwe kavu, paka mafuta ya nazi/au olive mara kwa mara katika mwili isipokuwa usoni, yanasaidia kulainisha ngozi na kuizuia isiendelee kutanuka.

Mazoezi ni muhimu husaidia kupunguza unene ambao husababisha kutokea kwa michirizi.

Vile vile kuzingatia lishe bora na Kunywa maji ya kutosha kila siku.




Toa maoni yako.



ZIJUE FAIDA ZA ASALI




image



Asali ni kitu kinachotumiwa na jamii nyingi toka zamani kwa matibabu (afya), ngozi (urembo) na mapishi sababu inasaidia vitu vingi. Ila leo tuangalie faida za kutumia asali kama dawa kwa mambo madogo madogo nyumbani;

  • Tiba ya Allergy
Asali inasaidia sana kuleta nafuu kama ukipata allergy yoyote iwe umekula au umeshika kitu kimekudhuru tumboni au kwenye ngozi, unaweza kulamba vijiko viwili vya asali au ukatia asali kwenye chai ukanywa, au kupaka kwenye ngozi inaleta nafuu.


  • Kuupa mwili nguvu
Asali kama ilivyo sukari inasaidia kuupa mwili nguvu ili uweze kujiendesha tofauti sukari ina madhara ukitumia sana tofauti na asali, hivyo ni vizuri kutumia asali badala ya sukari na ikafanya kazi ile ile bila kuleta madhara kwa afya yako.






  • kupunguza uzito
Ukitaka kupunguza uzito tumia asali kwenye chai za viungo asilia badala ya sukari kama tangawizi,mdalasini, limao, mchaichai itasaidia sana kupunguza uzito kwa haraka.

  • Kutibu kikohozi na matatizo ya koo 
 Unapokuwa na kikohozi au maumivu ya koo na hujapata dawa za hospitali iwe jaribu kula asali  iliyochanganywa na tangawizi iliyosagwa kiasi italeta nafuu, mtoto unaweza kumpa asali kijiko kidogo kimoja mara tatu
.
  • Kuondoa mba kichwani
Asali inasaidia kuondoa mba kwa. Nywele ambazo hazina wekwa relaxer, chukua asali vijiko 5 vya kulia chakula na changanya na vijiko vya maji 2 koroga vizuri, tia nywele maji zilowane kisha paka asali katika ngozi ya kichwa iache mpaka baada ya saa moja osha na maji ya uvuguvugu fanya hivyo mara mbili kila wiki kwa mwezi mzima mba wataisha.









Inashauriwa kutumia asali kwa kiasi hasa watu wenye kisukari, shinikizo la damu ni vizuri kupata ushauri wa daktari. Kama unajua faida nyingine za asali tueleze kwenye comments.