Tiba mbadala ya uzazi wa mpango
1. Papai
Mbegu za Papai pia ni dawa nzuri ya uzazi wa mpango kwa upande wa wanaume.
Zinachofanya mbegu za papai ni kupunguza idadi ya uwingi wa mbegu za
mwanaume (sperm count) na zinaweza kushuka mpaka kufika sifuri (zero
sperm count) na hivyo mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutungisha mimba.
Ukihitaji kuzaa tena unaacha tu kuzitumia na hali yako itarudi kama
kawaida. Kula mbegu za papai kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1
kila siku.
Unaweza kuanza zoezi hili wiki 3 kabla hujaamua rasmi kama ndiyo dawa yako ya uzazi wa mpango.
Watu wa bara la Asia wamekuwa wakitumia mbinu hii tangu miaka mingi iliyopita. Dawa hii haina madhara yoyote.
2. Mbegu za Nyonyo
Watafiti katika chuo kikuu cha Kano State College of Arts, Science
and Remedial Studies cha Nigeria wamethibitisha kuwa mbegu za nyonyo
zinaweza kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Mbegu za nyonyo
zinatumika kwa miaka mingi nchini India kama dawa ya uzazi wa mpango.
Unachotakiwa kufanya ni kunywa na maji mbegu 4 mpaka 5 kwa siku kila
siku wakati wa siku zako na zitakupa kinga ya uzazi wa mpango karibu kwa
mwaka mzima. Menya ganda lake la nje kabla ya kumeza.
Siku mbili au tatu za mwanzo za kutumia unaweza ukapatwa na
kutokujisikia vizuri, pumzi fupi, vipele (rashes), kizunguzungu kidogo,
kutapika au kuharisha nk lakini baadaye hali itatulia.
3. Tangawizi
Tangawizi huhamasisha kutokea kwa siku zako. Kunywa vikombe vitatu
mpaka vinne vya chai ya tangawizi kila siku ili kuzuia ujauzito. Chota
kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa tangawizi na uweke ndani ya
maji ya moto kikombe kimoja (robo lita/ml 250) na unywe yote (unaweza
kuongeza asali kidogo kupata ladha). Fanya zoezi hili kutwa mara 3 mpaka
mara 4 kwa siku 5 tangu ufanye tendo la ndoa bila kinga. Unaweza pia
kutumia tangawizi mbichi kwa matokeo mazuri zaidi.
4. Kotimiri (Parsley):
Kotimiri inapatikana kirahisi Dar Es Salaam na Zanzibar na ni kiungo
mhimu kwenye mahoteli mengi ya kitalii. Kunywa kikombe kimoja (robo
lita/ml 250) asubuhi na jioni cha chai iliyoandaliwa ukitumia kotimiri
mbichi kila siku ili kuzuia ujauzito usiotarajiwa. Hakuna madhara yoyote
mabaya ya matumizi ya dawa hii.
5. Vitamin C
Vitamini C ikitumika katika hali yake ya uasili kabisa inaweza
kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Kwenye vitamini C kuna ‘ascorbic
acid’ ambayo huzuia homoni inayouandaa mji wa uzazi (‘progesterone
hormone’) kushindwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo mimba kukosa
mahali pa kukaa baada ya yai kurutubishwa.
Meza viponge vya vitamini C mg 1500 mara mbili kwa siku mbili mpaka
tatu baada kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Vitamin C ni nzuri pia
kwa ngozi yako.
Mhimu:
1) Usitumie kiasi kingi sana cha vitamini C kwani
inaweza kupelekea mwili wako kutokuwa sawa au unaweza usijisikie vizuri
katika mwili wako.
2) Usitumie vitamini C kama unatumia dawa za kuzuia damu kuganda (anti-coagulant medications).
3) Usitumie vitamini C kama una tatizo la sickle cell (sikoseli).
Kumbuka kuwa makini mara zote, na wewe fanya utafiti binafsi pia.
Toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment