Thursday, February 3, 2022

FAIDA ZA TIKITI MAJI

 


Faida 7 za Matikiti Maji!!   

1) Kichangamsha ubongo!

Ndio! Umepatia! Tikiti maji huchangamsha ubongo kwasababu ya utajiri wa vitabini B6. Vitamini hii inaushawishi mkubwa katika ufanyaji kazi mzuri wa ubongo. Zaidi ya hayo uwepo wa maji kwenye tunda hili hulifanya kua chakula kizuri kwa ubongo ambao pia 85% ni maji


2) Ina utajiri wa Lycopini

Lycopini ni nini? Lazima utakua unajiuliza. Lycopini kemikali ambayo husaidia kuweka magonjwa mbali na wewe mfano magonjwa ya moyo, kansa, mototo wa jicho na hata asma! Najua utasikia ahueni kujua kua  tikiti maji lina Lycopini nyingi kuliko hata Nyanya.


3) Inaondoa Mawe

Ndio!! Kofia mbali na roho ya kupenda tunda hili. Ulaji wa Tikiti maji husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hata kukukinga figo zako zisipate  mawe hayo. Tunda hili lina utajiri wa maji, potassium, lycopene , Nitrik oxide ambazo hutunza figo zako. kwasababu ya asili yake ya majimaji, kula tunda hili husababisa kuongezeka kwa haja ndogo ambayo husaidia kuondoa mawe ambayo yanayeyushwa na potassium iliyo ndani ya tunda. Kwa hiyo kama unatatizo la mawe kwenye figo, usivunjike moyo, amua kula tikiti maji kuondoa mawe hayo.


4 ) Utajiri wa kufaa

Nina uhakika una kula tu ule mnofu wa ndani wa tunda. Lakini waulize wazee wa zamani kama walikula kwa mtindo huo. Hawakufanya hivyo kwa sababu matunda hayakua na kemikali zinazotokana na madawa. Sasa ukipata tikiti lililolimwa kienyeji jaribu kula maganda na mbegu zake kwasababu maganda ya tikiti yana citrulline, kemikali ambayo hugeuzwa na kua amino acid na kuimarisha kinga ya mwili na kuondoa sumu mwilini. 


Mbegu nazo zina viritubisho vya kutosha, zina kiasi kikubwa cha magnesiam, zink na protini. Tafuna mbegu kabla ya kumeza kupata virutubisho hivyo.


5) Habari njema kwa wanaume, tunda hili linawafanya kua vizuri kitandani. 

Titkiti maji pia huitwa Viagra ya asili kwa sababu inasifa ya kuongeza nguvu za kiume kama vile dawa zinavyofanya. Uwepo wa kemikali ya cirtrulline kwenye tikiti maji hubadilishwa na kua Argnine ambayo husaidia kutengeneza nitric oxide ambayo husaidia mtiririko wa damu na kuacha mishipa ya damu ikiwa mipana na hivyo kuzuia kupungua kwa nguvu za kiume. 


 6) Nzuri kwa Macho

Vitamini A inahitajika kwa wingi kwa afya ya macho yako na tunda hili linautajiri wa vitamin hiii. Kula gram 100 za tikiti kila siku kufanya macho yako yenye nguvu na afya.


 7 ) Inasaidia kupunguza uzito!

Matikiti maji yana kalori chache na maji mengi hivyo ni chakula kizuri kwa wale wanaotaka kupunguza uzito


No comments:

Post a Comment