Saturday, November 5, 2022

KUTOA MICHIRIZI MWILINI

 ) MAFUTA YA MNYONYO

Mafuta ya mnyonyo husaidia sana kwenye ngozi kama mikunjo ya ngozi husoni, chunusi, mabaka meusi kwenye ngozi lakini pia husaidia katika kuondoa michirizi.

stretch-marks-castor-500

  • paka mafuta ya mnyonyo mahala palipo kuwa na michirizi
  • funga eneo hilo kwa mfuko wa plastic kama uonavyo pichani
  • kisha weka kitu chenye joto juu ya mfuko huo kama heating pad au chupa ya maji ya moto kwa dakika ishirini (20) kila siku mpaka utakapo ona mabadiliko.

2)ALOE VERA husifika kwa kutibu magonjwa mbali mbali ya ngozi hivyo pia husaidia kuondoa michirizi hii ya ngozi kwa njia mbili zifuatazo,

Stretch-marks500

  • kwanza unaweza kupaka Aloe Vera tu na kuiacha ikae kwenye sehemu iliyo kuwa na michirizi kwa dakika 15 kisha uoshe kwa maji ya vuguvugu au,
  • njia ya pili, ni kuchanganya majimaji ya Vitamin A, Vitamin E na Aloe Vera yenyewe kisha paka kwenye eneo lililo athirika na michirizi kila siku. Paka kama mafuta ya kupakaa mwilini.

3)SUKARI

Stretch-Marks-Sugar-Almond-Oil-Lemon-600x450

  • Chukua sukari mbichi kijiko kimoja, mafuta ya Almond na  Maji maji ya ndimu, changanya kwa pamoja halafu paka pale palipo athirika
  • Fanya hivi kila siku kabla ya kwenda kuoga, fanya kwa mwezi mzima na utaona matokeo yake.

4) JUISI YA VIAZI vina vitamini na madini ambayo kukuza ukuaji wa seli za ngozi.

Potatoes

  • kata kata kiazi chako katika vipande vyembamba
  • chukua kipande cha kiazi na ukisugue pale kwenye michirizi yako hakikisha yale maji ya viazi yame ingia kwenye michirizi ako.
  • kaa nayo kwa muda na kisha uondoe kwa maji ya uvugu vugu.

Wednesday, October 12, 2022

Faida za stafeli

 

FAIDA ZA TUNDA LA STAFELI (TOPE TOPE)

Stafeli lina virutubisho vingi, baadhi yake ni AMINO ACID, ACETOGENINC, VITAMIN C, IRON, PHOSPHORUS, CALCIUM, NIACIN, RIBOFLAVIN na vingine vingi.

1. HUSAIDIA KUTIBU SARATANI

Ingawa sio tiba ya moja kwa moja kwa saratani, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani.

Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa wagonjwa wa saratani njia nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya mionzi na kupata ahueni kubwa.

UCHUNGUZI WA WATAALAM

Zaidi ya majaribio 15 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:

  • Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo n.k.
  • Stafeli lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika kutibu aina mbalimbali ya saratani.
  • Mchanganyiko wa virutubisho vya ‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huuwa seli zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.
  • Stafeli hudhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.
2. HUSAIDIA MAUMIVU YA KIPANDA USO

Miongoni mwa virutubisho vilivyomo katika tunda hili ni pamoja na 'Riboflavin' husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda uso.

3. HUZUIA ANEMIA (Ugonjwa wa kukauka damu)

Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini.

4. HUTIBU MAGONJWA YA INI

Ukiachana na ladha tamu ya juisi ya stafeli lakini pia inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.

5. KUIMARISHA MIFUPA

Stafeli ni chanzo kizuri pia cha madini ya kopa (copper) na kalshiamu (calcium), virutubisho ambavyo huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.

Matatizo mengine yanayoweza kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye ‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.

FAIDA NYINGINE ZA STAFELI (Kwa ufupi)

• Hutumika kutibu maumivu ya nyuma ya mgongo ( low back pain )

• Mstafeli hutumika kutibu maumivu ya jongo/gout

• Hurekebisha usawa wa kiasi cha damu na sukari mwilini.

• Huongeza kinga ya mwilini

• Hudhibiti ukuaji wa bacteria, virusi, vijidudu nyemelezi na uvimbe.

• Huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka unapokuwa mgonjwa.

• Hutibu jipu na uvimbe.

• Hukimbiza chawa.

MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA

Mbali ya tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu, vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani, mbegu na magamba yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:
  • Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.
  • Maji ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika kushusha kiwango cha sukari mwilini.
  • Mbegu zake hutengenezwa dawa ya kula na kufukuza wadudu waharibifu.
  • Majani ya mti wa mstafeli hutumika kutibu maumivu ya mishipa. Saga majani yake mpaka yalainike kabisa, kasha paka taratibu eneo la mishipa lililo na maumivu mara mbili kwa siku.
  • Ni tiba ya asili ya maumivu ya mishipa, yasage majani yake mpaka yalainike kabisa kisha paka taratibu eneo la mshipa lililo na maumivu mara mbili kwa siku
  • Huongeza kinga ya mwili
  • Hutibu jipu na uvimbe

TAHADHARI
Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka (hypotension or hypertension). Hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate ushauri wa daktari kwanza.

Lakini pia stafeli kwa asili yake lina kiasi kingi cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.

Thursday, February 3, 2022

FAIDA ZA KUVUTA BANGI

 FAHAMU FAIDA NANE ZA KUVUTA BANGI, inakufanya uwe mbunifu 


1. Huzuia kuenea kwa kansa ya MATITI kwa wanawake 


2. Huongeza nguvu za Kiume na ubora wa Manii. Kwa mujibu wa utafiti wa chuo cha Harvard Marekani.


3. Huondoa wasiwasi na kukufanya uwe jasiri.


4. Hutibu Presha ya Jicho


5. Inasaidia kuzuia  Kifafa 


6. Huongeza uwezo wa kubuni (Creativity) 


7. Inaboresha afya ya mapafu na kupunguza athari za tumbaku katika mapafu.


8. Huboresha ngozi na kuchangamsha kazi za mwilini.


ANGALIZO. Matumizi ya kiafya ya bangi yanapaswa kuwa chini ya Wataalamu. Kwa kuwa athari zake hutegemea kiasi cha matumizi na hali ya afya ya mtumiaji.

FAIDA ZA KARAFUU

 

Faida za Mafuta ya karafuu



Karafuu kwa jina la kisayansi (Syzygium aromaticum) ni kiungo chenye harufu nzuri ambacho kimekuwa kikitumika na jamii ya watu mbalimbali kwa miaka mingi duniani kote. Leo utajifunza faida pia za mafuta ya karafuu.

Kama ilivyo kwa viungo vingine mmea wa karafuu pia unaweza kutengeneza mafuta tiba ambayo yanaweza kutibu changamoto nyingi za kiafya. Ni mafuta ambayo hutakiwi kuyakosa nyumbani kwako muda wote. Nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa karafuu ni pamoja na Indonesia, india, Zanzibar pamoja na Madagascar.

Faida na Matumizi ya Mafuta ya Karafuu.

  • Kutibu magonjwa ya meno kama kuvimba fizi na maumivu makali ya meno
  • Mfumo wa chakula: mafuta ya karafuu yanasaidia kutuliza misuli ya tumbo na hivo kuleta nafuu kwa changamoto za kutapika na tumbo kuchafuka.
  • Kwenye ngozi: mafuta yanasaidia kutibu changamoto za chunusi, makovu kwenye ngozi na vigwaru/masundosundo.
  • Kwenye mfumo wa hewa; mafuta yakitumika huleta nafuu kwa mwenye kikohozi kikali, pumu ,TB, pamoja na kufungua njia za hewa.
  • Kuua vimelea wabaya na hivo kusaidia mweye fangasi, vidonda na majeraha kupona mapema.
  • Marashi: kutokana na harufu yake nzuri mafuta ya karafuu yanatumika kutengeneza pafyumu .
  • Kiungo cha chakula; ili kuongeza ladha karafuu inatumika kwenye chakula .
  • Mafuta ya karafuu pia hutumika kwa masaji ya mwili ili kuondoa maumivu .

Namna ya Kutumia Mafuta ya Karafuu

  • Kwa changamoto za upumuaji chemsha maji kidogo weka mafuta ya karafuu kisha vuta mvuke wake.
  • Chovya kiasi kodogo cha mafuta pakaa kwenye ngozi ili kuweka ngozi nyororo
  • Kwa maumivu ya jino. chukua kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu, changanya na kiasi kidogo cha mafuta ya nazi kisha fanya masaji kwenye eneo la jino lililoathirika.
  • Kwa maumivu ya kichwa chovya kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu kisha sugua eneo la mbele la kichwa kwa muda wa dakika 5
  • Mafuta ya karafuu pia yanaweza kutumika kufukuza wadudu kama mbu endapo utajipaka kwenye ngozi.
  • Kuondoa harufu mbaya ndani ya nyumba unaweza kuchanganya mafuta kiasi kwenye sufuria weka na maji kiasi kidogo, kisha chemsha maji katika moto mdogo taratibu mvuke utasambaa ndani ya nyumba na kuleta harufu nzuri.

Je Mafuta ya Karafuu ni Salama kutumiwa na kila mtu?

Kama ilivyo kwa mafuta tiba mengine,mafuta ya karafuu yanatakiwa kutumika kwa uangalifu kwani kiwango kikubwa kinaweza kuleta athari kwenye mwili, tahadhari zaidi ichukuliwe unapopakaa mafuta kwenye maeneo kama kwenye fizi.

Wanawake wajawazito na wenye mimba wanaweza kutumia karafuu kwenye chakula, lakini siyo salama kutumia mafuta ya karafuu yenyewe.
Watoto wadogo chini ya miaka miwili wasitumie mafuta ya karafuu kwani yaweza kupelekea kuathirika kwa baadhi ya viungo vya mwili.

Kama umepangiwa kufanyiwa upasuaji inashauriwa usitumie mafuta ya karafuu week mbili kabla, kwani kampaundi ya eugenol iliyopo kwenye mafuta ya karafuu husababisha kuchelewa kupona kidonda.

FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU




 ZIJUE FAIDA,MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

 


               

MAGONJWA YANAYOTIBIKA KUPITIA KITUNGUU SAUMU

Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)

Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I

Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine

Huzuia kuhara damu (Dysentery)

Huondoa Gesi tumboni

Hutibu msokoto wa tumbo

Hutibu Typhoid

Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi

Hutibu mafua na malaria

Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)

Hutibu kipindupindu

Hutibu upele

Huvunjavunja mawe katika figo

Hutibu mba kichwani

Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.

Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu

Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)

Hutibu maumivu ya kichwa

Hutibu kizunguzungu

Hutibu shinikizo la juu la damu

Huzuia saratani/kansa

Hutibu maumivu ya jongo/gout

Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Huongeza hamu ya kula

Huzuia damu kuganda

Husaidia kutibu kisukari

Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi

Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu


FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.

Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.


MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU


Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji

Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)

Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha

Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.

Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.

Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.

Kumbuka:                                                                                                                                  

kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.

FAIDA ZA TIKITI MAJI

 


Faida 7 za Matikiti Maji!!   

1) Kichangamsha ubongo!

Ndio! Umepatia! Tikiti maji huchangamsha ubongo kwasababu ya utajiri wa vitabini B6. Vitamini hii inaushawishi mkubwa katika ufanyaji kazi mzuri wa ubongo. Zaidi ya hayo uwepo wa maji kwenye tunda hili hulifanya kua chakula kizuri kwa ubongo ambao pia 85% ni maji


2) Ina utajiri wa Lycopini

Lycopini ni nini? Lazima utakua unajiuliza. Lycopini kemikali ambayo husaidia kuweka magonjwa mbali na wewe mfano magonjwa ya moyo, kansa, mototo wa jicho na hata asma! Najua utasikia ahueni kujua kua  tikiti maji lina Lycopini nyingi kuliko hata Nyanya.


3) Inaondoa Mawe

Ndio!! Kofia mbali na roho ya kupenda tunda hili. Ulaji wa Tikiti maji husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hata kukukinga figo zako zisipate  mawe hayo. Tunda hili lina utajiri wa maji, potassium, lycopene , Nitrik oxide ambazo hutunza figo zako. kwasababu ya asili yake ya majimaji, kula tunda hili husababisa kuongezeka kwa haja ndogo ambayo husaidia kuondoa mawe ambayo yanayeyushwa na potassium iliyo ndani ya tunda. Kwa hiyo kama unatatizo la mawe kwenye figo, usivunjike moyo, amua kula tikiti maji kuondoa mawe hayo.


4 ) Utajiri wa kufaa

Nina uhakika una kula tu ule mnofu wa ndani wa tunda. Lakini waulize wazee wa zamani kama walikula kwa mtindo huo. Hawakufanya hivyo kwa sababu matunda hayakua na kemikali zinazotokana na madawa. Sasa ukipata tikiti lililolimwa kienyeji jaribu kula maganda na mbegu zake kwasababu maganda ya tikiti yana citrulline, kemikali ambayo hugeuzwa na kua amino acid na kuimarisha kinga ya mwili na kuondoa sumu mwilini. 


Mbegu nazo zina viritubisho vya kutosha, zina kiasi kikubwa cha magnesiam, zink na protini. Tafuna mbegu kabla ya kumeza kupata virutubisho hivyo.


5) Habari njema kwa wanaume, tunda hili linawafanya kua vizuri kitandani. 

Titkiti maji pia huitwa Viagra ya asili kwa sababu inasifa ya kuongeza nguvu za kiume kama vile dawa zinavyofanya. Uwepo wa kemikali ya cirtrulline kwenye tikiti maji hubadilishwa na kua Argnine ambayo husaidia kutengeneza nitric oxide ambayo husaidia mtiririko wa damu na kuacha mishipa ya damu ikiwa mipana na hivyo kuzuia kupungua kwa nguvu za kiume. 


 6) Nzuri kwa Macho

Vitamini A inahitajika kwa wingi kwa afya ya macho yako na tunda hili linautajiri wa vitamin hiii. Kula gram 100 za tikiti kila siku kufanya macho yako yenye nguvu na afya.


 7 ) Inasaidia kupunguza uzito!

Matikiti maji yana kalori chache na maji mengi hivyo ni chakula kizuri kwa wale wanaotaka kupunguza uzito


Monday, January 31, 2022

Faida za ndimu/limao

 Maajabu Ya Ndimu/Limao.



 

 

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Asubuhi

Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini, lakini kunywa maji vuguvugu yenye ndimu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku.

Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili, ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).

Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu, wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na ladha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na leo tutaziangazia faida 11 muhimu.

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu.

#1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni.

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

#2: Huboresha Kinga za Mwili.

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

#3: Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini.

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

#4: Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani.

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

#5: Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi.

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

#6: Usafishaji wa Mwili na Damu.

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

#7: Kurekebisha Sukari katika Mwili.

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

#8: Dawa ya Kikohozi na Mafua.

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

#9: Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu.

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

#10: Husaidia Kupungua Uzito.

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale ambao wanataka kupungua uzito.

#11: Kuondoa Harufu ya Mdomo.

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

Anza Siku Kwa Kunywa Maji yenye Ndimu Kila Siku.

Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula kitu chochote kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako.