Monday, January 31, 2022

Faida za ndimu/limao

 Maajabu Ya Ndimu/Limao.



 

 

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Asubuhi

Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini, lakini kunywa maji vuguvugu yenye ndimu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku.

Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili, ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).

Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu, wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na ladha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na leo tutaziangazia faida 11 muhimu.

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu.

#1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni.

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

#2: Huboresha Kinga za Mwili.

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

#3: Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini.

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

#4: Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani.

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

#5: Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi.

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

#6: Usafishaji wa Mwili na Damu.

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

#7: Kurekebisha Sukari katika Mwili.

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

#8: Dawa ya Kikohozi na Mafua.

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

#9: Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu.

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

#10: Husaidia Kupungua Uzito.

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale ambao wanataka kupungua uzito.

#11: Kuondoa Harufu ya Mdomo.

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

Anza Siku Kwa Kunywa Maji yenye Ndimu Kila Siku.

Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula kitu chochote kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako.

FAIDA ZA KAROTI

 FAIDA YA KULA KAROTI KWA AFYA YA MWILI WAKO

 

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti kama kiungo na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi


Faida ya kula karoti ni kama zifuatazo


i. Karoti husaidia kuimarisha macho kuona vizuri, mfano tatizo la kutoona vizuri usiku, pia inasaidia kuondoa matatizo ya allergy kwenye macho mfano macho kuwasha sababu ya vumbi.

Karoti inarutubisha cells mwilini na kuzifanya zisizeeke haraka. Hii inatokana na  uwepo wa Vitamin A ambayo ni muhimu katikakuimarisha uwezo wa macho kuona.

ii. Huifanya ngozi iwe nzui na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nazi au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka, ukimaliza acha kama dakika 15 na zaidi kisha oga, itasaidia kuondoa taka katika vinyweleo, kuifanya ngozi iwe laini na kuondoa mikunjo katika ngozi, Kumbuka inatakiwa asali mbichi na siyo asali yoyote.

iii. Karoti husaidia kuondoa sumu na taka mwilini, inaondoa mafuta yasiyotakiwa katika ini (cholesterol) na kuliwezesha lifanye kazi vizui, Kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri (kuzuia constipation).

iv. Karoti zinasaidia kufanya fizi na meno kuwa imara na kuchochea uzalishwaji wa mate.

v. Pia inasaidia kuzuia stroke (kiharusi, baadhi ya watafiti kutoka vyuo vikuu duniani wanasema  ulaji wa karoti sita kwa wiki husaidia kutopata stroke.

Pia imegundulika kuwa karoti zinatibu tatizo la kupoteza kumbukumbu kwa wazee.

iv. Karoti hupunguza hatari ya kupata Shinikizo la Damu (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (bllod vessels na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).

v. Karoti pia husasidia kuzuia magonjwa mengine kama vile kisukari (Diabetes), Kiharusi (Stroke), Kansa pamoja na magonjwa ya moyo.

vi. Karoti husaidia kuongeza kinga mwilini (immune booster). Kwasababu tabaia asilia ya karoti ni kuwa na antibacteia pamoja na antiseptic ambazo husaidia kuongeza kinga za mwili. Pia Karoti ina Vitamin C muhimu kwa kusisimua seli nyeupe za damu (white blood cells) ambazo ni sehemu muhimu katika kinga ya mwili.


Sunday, January 30, 2022

FAIDA ZA TANGAWIZI

 FAIDA 48 ZA TANGAWIZI MWILINI;


wengi wetu tumekua tukitumia tamgawizi kama kiungo kwenye vyakula mbalimbali hasa chai lakini hatukuweza kujua faida zake upande wa afya zetu.

Tafiti kadha wa kadha zimefanyika na zimeainisha yafuatayo juu ya matumizi ya tangawizi. 


1. Huondoa sumu mwilini haraka sana


2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi


3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi


4. Huondoa uvimbe mwilini


5. Huondoa msongamano mapafuni


6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake


7. Huondoa maumivu ya koo


8. Huua virusi wa homa


9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini


10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)


11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.


12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”


13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)


14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)


15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)


16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo


17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi

18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi


19. Huongeza msukumo wa damu


20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo


21. Huzuia damu kuganda


22. Hushusha kolesto


23. Husafisha damu


24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa


25. Hutibu shinikizo la juu la damu


26. Husafisha utumbo mpana


27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma


28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI


29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula


30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu


31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu


32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa


33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula


34. Husaidia kuzuia kuharisha


35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu


36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto


37. Hutibu homa ya kichwa


38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi


39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito


40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)


41. Huimarisha afya ya figo


42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi


43. Ina madini ya potassium ya kutosha


44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.


45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha


46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium


47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene


48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita. 


FAIDA ZA NDIZI MBIVU

 UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO

UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO : Naam. Baada ya kusoma makala hii hutaiangalia ndizi tena kwa mtaazamo uleule uliozoea

• Ndizi imejumuisha aina tatu za sukari ya asili ambazo ni glukosi, sukrosi na fruktosi.

• Ndizi hutoa nishati muhimu, ya kudumu na ya kutumika wakati wowote mwilini.

• Utafiti umethibitisha kwamba ndizi mbili tu zinatosha kuzalisha nishati ya kuufanya mwili ufanye kazi ngumu kwa dakika tisini. Hakuna shaka ndizi ndiyo kipenzi namba moja kwa wanariadha wanaoongoza duniani.

• Lakini nishati siyo pekee ambacho ndizi yaweza kutupatia nguvu ili kuilinda afya yetu. Pia inaweza kutusaidia kukabiliana au kutulinda dhidi ya magonjwa sita. Hizi ndizo zinazofanya ndizi kuwa muhimu katika mchanganyiko wa milo yetu ya kila siku.

 

MIONGONI MWA FAIDA ZA KULA NDIZI:

KULETA RAHA: Kutokana na utafiti uliowahi kufanyika, watu wenye matatizo au ukosefu wa raha maishani, wamejiona wakirudia furaha waliyokuwa nayo awali baada ya kula ndizi. Hii ni kwa sababu ndizi ina aina ya protini ijulikanayo kitaalam kama tryptophan ambayo mwili wetu huibadilisha na kuwa serotonin, ambayo hukufanya ujisikie mwenye furaha.

VITAMINI B6 iliyopo kwenye ndizi husaidia kurekebisha glukosi iliyopo kwenye damu na hivyo kuboresha hali ya mwili na kukufanya ujisikie vizuri.

ANEMIA: Ndizi pia ina kiasi kingi cha madini ya chuma ambayo husaidia kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu, hivyo husaidia mwili kujikinga dhidi ya maradhi mbalimbali, kama anemia.

 

Tafiti za Sehemu mbalimbali zimethibitisha uwezo wa ndizi kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya.

SHINIKIZO LA DAMU: Tunda hili lina kiasi kikubwa cha madini ya potasi na kiasi kidogo cha chumvi na kuifanya kuwa bora katika kudhibiti maradhi ya shinikizo la damu. Hii imethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.

UWEZO WA KIAKILI: Ushahidi unaonyesha kwamba takribani wanafunzi 200 huko Marekani walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi wakati wa kufungua kinywa na mlo wa mchana. Hii ina maana kwamba huongeza uwezo wao kiakili. Kichocheo kikubwa cha kupata akili ni madini aina ya potasi yaliyomo.

KUVIMBIWA: Kambakamba za protini zilizomo kwenye ndizi zinasaidia kuzabua tindikali (antiacid). Hivyo kama mtu ana tatizo la kiungulila ajaribu kutumia ndizi ili kupata nafuu. Aidha ndizi husaidia kurejesha hali ya utendaji kazi wa kawaida wa tumboni. Ikiwemo kudhibiti kuvimbiwa bila kutumia kemikali.

KUHARISHA: Kula ndizi mbivu tatu kubwa na huzuia aina nyingi za miharisho na msokoto wa tumbo.

MAUMIVU YA KICHWA: Moja ya njia nyepesi na ya haraka ya kukabiliana na maumivu ya kichwa ni kwa kula ndizi iliyosagwa na kuchanganywa na maziwa. Hii husaidia kusawazisha sukari ya ziada kwenye damu.

Wataalam wamethibitisha kwamba kiafya ndizi ni tunda bora zaidi ya mengine .

Kusaidia mwili kuwa katika hali nzuri wakati wote. Wakati ikifanya hivyo vilevile hurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini.

HOMA NA UCHOVU WA ASUBUHI: Ulaji wa mara kwa mara wa ndizi husaidia kuongeza sukari mwilini, hivyo kuondoa hali ya homahoma na uchovu.

KUUMWA NA MBU: Kabla kutumia krimu kusugua sehemu yenye maumivu ya kuumwa na mbu, jaribu kutumia ndizi mbivu. Utashangazwa na matokeo yake.

KUONGEZEKA UZITO: Uchunguzi uliofanya katika Chuo cha Mambo ya Saikolojia nchini Australia, ulibaini kwamba shinikizo la kazi huchochea watu wengi kula vyakula kama chokoleti na mikaango mbalimbali. Ulitafiti kwenye wagonjwa 500 waliolazwa hospitalini, ulionyesha kwamba wengi wana vitambi na kutokana na kazi zenye shinikizo kubwa. Uchunguzi ukahitimisha kwamba watu wajihadhari na vyakula vinavyochochea mifadhaiko ya akili. Hivyo ikapendekezwa kula zaidi vyakula vya wanga. Ambavyo hupunguza kiwango cha sukari mwilini.

VIDONDA VYA TUMBO: Ndizi hutumika kama mlo kwa wagonjwa wenye matatizo haya kwa sababu ya ulaini wake. Ndizi mbichi za kupika ndizo zifaazo hapa. Hizi husaidia kupunguza tindikali ya ziada tumboni, pia kusambaa kwenye kuta za tumbo na hupunguza maumivu.

UDHIBITI WA JOTO LA MWILI: Tamaduni nyingi zinakubali kwamba ndizi ni kipoozi cha joto la mwili ambalo husababisha na hali mbalimbali zisizo za kawaida mwilini. Mathalani huko Thailand akina mama waja wazito hutumia ndizi kuhakikisha watoto wanaowazaa wanakuwa katika hali nzuri na ya ubaridi.

UVUTAJI TUMBAKU: Ndizi huwasaidia watu wanaojaribu kuacha kuvuta tumbaku. Vitamini B6 na B12, potassium na maginesiam ipatikanayo kwenye tunda hili husaidia kuondoa athari ya sumu iitwayo nikotini.

UCHOVU: Madini ya potasi yaliyo kwenye ndizi husaidia kutuliza mapigo ya moyo na kuwa ya kawaida. Hupeleka hewa safi kwenye ubongo na kurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini. Wakati tukiwa wachovu kiwango cha utendaji kazi wa mifumo mbalimbali ya mwili huongezeka na hivyo hupunguza kiasi cha potasi mwilini, upungufu huu hufidiwa kwa kula ndizi mara kwa mara.

HITIMISHO: Hivyo ndizi ni dawa ya kuponya maradhi mbalimbali. Aidha zina utajiri mkubwa wa protini mara nne zaidi, mara mbili zaidi ya wanga, mara tatu zaidi ya madini ya fasifarasi, mara tano zaidi ya vitamini A na madini ya chuma, ukilinganisha na aina zingine za vyakula. Pengine ni wakati muafaka kuzingatia msemo “kula ndizi kila siku kuepuka kuonana na daktari.

Saturday, January 29, 2022

SEVEN RULES OF LIFE

 1...let it go

2...ignore them

3...give it time

4... don't compare to others

5...stay calm

6... it's on you

7...smile

If you love it comment below.....